Kiongozi wa shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ameuawa maafisa nchini Somalia wanasema.
Serikali ya Kenya imesema kuwa Mohamed Kuno ndiye aliyepanga njama za shambulio hilo la mwezi Aprili 2015 ambapo takriban watu 148 waliuawa.
Vikosi vya Somalia vinasema kuwa ni miongoni mwa watu 16 waliouawa katika shambulio la usiku katika msafara wa magari mjini Kismayu ,mji wa Bandari uliopo kusini mwa Somalia.
Wanne ya wale waliouawa waliripotiwa kuwa maafisa wandamizi wa wapiganaji wa al-Shabab.
Mwandishi wa maswala ya usalama wa BBC barani Afrika Tomi Oladipo amesema kuwa habari hizo ni mafanikio makubwa kwa Somalia na washirika wake katika vita dhidi ya Alshabab.
Post a Comment