Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ameahidi kuwa ataendelea na mpango wa kuwasamehe washambuliaji katika eneo la mafuta la Niger Delta.
Katika hotuba ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wake, Rais Buhari amesema, mashambulio ya karibuni katika eneo hilo,hayatoizuia serikali yake, kushauriana na viongozi wa jamii, ili kushughulikia malalamiko ya watu.
Alisema, mpango wa msamaha, ambao ulitarajiwa kumalizika mwisho wa mwaka ujao, unaweza kuendelezwa.
Wanasiasa na wapiganaji wa eneo la mdomo wa Mto Niger, wamelalamika kuwa jamii za Niger Delta, zinastahiki kupewa utajiri unaotoka eneo lao, na wanataka uchafu kutoka visima vya mafuta, usafishwe.
Post a Comment