0

Klabu ya Manchester City imemsajili kiungo wa kati wa Ujerumani IIkay Gundogan kutoka kwa kilabu ya Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka minne.
Mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye hatoshiriki katika michuano ya Euro 2016 pamoja na kuanza kwa ligi ya Uingereza msimu huu kutokana na jeraha atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa kilabu ya Mancity Pep Guardiola.
Manchester City imeripoti kulipa kitita cha pauni milioni 20 kumpata Gundogan.
'Nilipogundua kwamba City walikuwa wakinihitaji,moyo wangu ulikubali'',alsiema.''Mambo yamenda haraka sana''.
Mkurugnzi wa klabu hiyo ya Ligi ya Uingereza Txiki Begiristain alipongeza maadili ya Gundogan pamoja na uwezo wake

Post a Comment

 
Top