0
Wanajeshi wa serikali nchini Iraq wanaendelea na mikakati wa kuuteka mji wa Fallujah huku wapiganaji wa Islamic State wakiendesha mashambulizi makubwa katika mji ulio Kaskazini mwa mto Eupharates.
Taarifa zinasema kuwa idadi kubwa ya washambualiaji wa kujitoa mhanga wa Islamic State waliingai mji wa Hit baada ya kuafanya mashambulizi ya roketi.
Image copyrightAFP
Wilaya nyingi za mji wa Hit sasa zinaripotiwa kuwa chini ya udhibiti wa Islamic State huku familia nyingi zikiondoka mji huo.
Vikosi vya serikali na wapiganaji wa makabila wanajibu mashambulizi hayo. Waliuteka mji wa Hit kutoka kwa Islamic State mwezi uliopita.

Post a Comment

 
Top