Benki kuu ya Uingereza imetangaza kuzinduliwa kwa noti za Plastiki za pauni 5.
Noti hiyo ya pauni tano itakuwa ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo sarafu ya nchi hiyo imekuwa ikichapishwa kwenye karatasi.
Plastiki hiyo inayofahamika kwa jina halisi 'polymer' ni nyepesi na itahitaji wino maalum kutumiwa kuchapishwa pande zote mbili.
Hata hivyo Uingereza sio taifa la kwanza kutumia noti za plastiki, mataifa mengine zaidi ya 20 duniani tayari yanatumia noti zilizotengezwa kutokana na plastiki.
Mataifa hayo ni pamoja na Scotland, Australia, New Zealand, na Canada
Benki kuu ya Uingereza inasema kuwa noti za plastiki (Polymer) ni bora kuliko zinazotumika sasa za karatasi kwa sababu zinadumu zaidi na pia hazichafuki.
Aidha noti hizo hazilowi maji haswa pale mtu anaposahau pesa mfukoni kisha nguo zake zikaoshwa.
Benki hiyo pia inasema kuwa ni vigumu mno mtu kutengeneza noti bandia za plastiki.
Pia benki hiyo inasema kuwa noti za plastiki zitapunguza gharama ya kuchapisha noti mpya kila mwaka.
Noti hiyo itaanza kutumika mwezi septemba mwaka huu.
Baada ya majaribio ya noti ya pauni tano, benki hiyo inapania kuzindua noti za pauni 10 mwakani na kisha pauni 20 kufikia mwaka wa 2020.
Post a Comment