0
NUSU ya wakulima nchini wanatajwa kuwa ndio wanatumia simu za mkononi, kufanya miamala mbalimbali ya fedha na kutafutia masoko ya mazao yao.
Hayo yalielezwa wakati wa kuwasilisha matokeo ya utafiti kuhusu namna familia za wakulima wadogo, zinavyosimamia mapato yao na kukabili matatizo mbalimbali ya kifedha.
Utafiti huo ulifanywa na Taasisi ya kimataifa ya ushirikishwaji wa kifedha (CGAP) ikishirikiana na Mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania (FSDT).
Mkuu wa Kitengo cha Kilimo na Huduma za Fedha wa FSDT, Mwembeki Baregu, alisema jana kuwa kutokana na wakulima wengi kutotumia simu za mkononi kwa manufaa ya kiuchumi, wameamua kuzishirikisha kampuni za simu kwenye mjadala wa kujadili matokeo hayo ya utafiti ili waeleze namna gani watawasaidia wakulima wajue umuhimu wa kusaka masoko kwa kutumia simu za mkononi.

Post a Comment

 
Top