0
Waziri wa utamaduni nchini Iran anasema kuwa nchi hiyo haitawatuma raia wake kwenda kuhiji mwaka huu nchini Saudi Arabia.
Ali Jannati alisema kuwa sio vizuri kwa Saudi Arabia kuwawekea vizuizi raia wa Iran wanaotaka kuhiji.
Image copyrightAFP
Image captionMamia ya watu waliuawa kwenye mkanyagano mwaka uliopita
Wakati wa hija ya mwaka uliopita, mamia ya mahujaji waliuawa wengi wao raia wa Iran wakati wa kisa kibaya cha mkanyagano.
Msukosuko kati ya Iran na Saudi Arabia umekuwa ukiongezeka wakati pande hizo mbili zinaunga mkono makundi tofauti yanayopigana nchini Syria na Yemen.

Post a Comment

 
Top