Zogo limezuka kati ya waandalizi wa mashindano ya gofu duniani, PGA Tour na mgombea wa urais wa chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump.
Waandaji wa mashindano hayo PGA Tour wanasema kuwa hawajakusanya pesa za kutosha za kugharamia mashindano hayo katika uwanja wa bwana Trump wa Doral ulioko Miami mwakani.
Kwa hivyo wamesema watayahamishia hadi Mexico City.
Bwana Trump amesema kuwa waandaaji wa mashindano hayo wametoa kipao mbele swala la faida na kupuuza umuhimu wa ajira kwa maelfu ya raia wa Marekani.
Katika mikutano yake ya kampeni ametaja Mexico kama taifa linalohujumu uchumi wa Marekani na tayari amewahi kunukuliwa akitaja wahamiaji kutoka Mexico kama wabakaji na wauaji.
Mkurugenzi wa PGA Tour Timothy Finchem ameiambia BBC kuwa matamshi na hadhi aliyopewa bwana Mr Trump wakati huu inahujumu juhudi zake za kutafuta mdhamini wa mashindano hayo.
''Kimsingi ni swala la udhamini, hatuma udhamini'' alisema bwana Finchem.
Mmoja wa wadhamini wakuu wa mashindano hayo ya gofu, kampuni ya kutengeneza magari ya Cadillac haijaandikisha mkataba mpya kama ilivyokuwa ikitarajiwa.
"Donald Trump kwa sasa ni nembo kubwa sana ,na pindi unapojaribu kushawishi kampuni kudhamini mashindano naye afahamu kuwa Trump atakuwepo hiyo inamaanisha kuwa watagawana ushawishi na Trump''.
''Ukizingatia mamilioni ya dola inayotajwa utaona kwanini mashirika mengi yanasusia kudhamini mashindano hayo'' alisema bwana Finchem.
Trump kwa upande wake anasema kuwa ni siku mbaya sana katika historia ya Miami.
''Hii ni siku ya huzuni sana Miami na kwa mchezo wa gofu nchini Marekani'' alisema Trump
Mashindano hayo sasa yataandaliwa katika klabu ya Club de Golf Chapultapec viungani mwa jiji la Mexico City
Post a Comment