Mwanamume mmoja raia wa Gambia alikufa maji huku watu wakitazaka katika eneo la Venice's Grand Canal nchini Italia.
Gazeti la Times la nchi hiyo linasema kuwa watu katika mji huo walipiga picha kisa hicho huku wakicheka na kumtupia maneno ya ubaguzi wa rangi Pateh Sabally mwenye umri wa miaka 22.
"Endelea, rudi nyumbani," mmoja wao aliongea kwa sauti.
Kulingana na shirika la Reuters, majaji nchini Italia wameanzisha uchunguzi baada ya video iliyonaswa kwa kutumia simu ya mkoni siku ya Jumapili kuchapishwa kwenye mitandao.
Hakuna mtu aliyejaribu kuruka kwenye maji hayo yenye baridi kumsaidia bwana Sebally, ambaye anaripotiwa kuwasili nchini Italia miaka miwli iliyopita.
Lakini vifaa vya kuokoa maisha viliruswa kwenye maji karibu na mahala alikuwa laniki hakuonekana kuvifikia, na kuzua uvumi kuwa alikuwa anataka kujiua.
"Yeye ni mjinga, anataka afe," mtu anasikika akiongea kwenye video hiyo.
Zaidi ya wahamiaji 181,000 waliwasili Italia kwa mashua mwaka 2016 wengi kutoka nchi za Afrika ambalo ni ongezeko la karibu asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Post a Comment