MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco, juzi Jumamosi alishindwa kuonyesha makeke yake mbele ya beki wa kati wa Azam, Agrey Morris, ambapo beki huyo amefunguka kuwa alijipanga
kisawasawa kukabiliana naye.
Bocco amejiunga na Simba akitokea Azam kwa mkataba wa miaka miwili na juzi ilikuwa mechi yake ya kwanza ya ligi kucheza dhidi ya timu yake ya zamani kwenye Uwanja wa Azam Complex. Katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu, Bocco alipata wakati mgumu wa kufunga kutokana na ugumu alioupata kutoka kwa beki huyo akisaidiwa na Mghana, Yakubu Mohammed.
Morris ameliambia Championi Jumatatu kuwa sababu kubwa ya kuweza kumdhibiti mshambuliaji huyo ni kwa kuwa walijipanga kukabiliana naye, yeye pamoja na washambuliaji wengine wa timu hiyo. “Nadhani Bocco hakuweza kufunga kwa sababu nilijipanga na wenzangu pia walifanya hivyo maana kawaida kila mshambuliaji hupambana kufunga na beki kazi yake ni kuzuia. “Sasa katika suala la Bocco, yeye alikuwa anapambana atufunge kama mshambuliaji lakini sisi nao tulikuwa tunapambana kuhakikisha hafungi kama mabeki na ndicho kilichotokea,” alisema Morris.
Post a Comment