PHONE NO:+255624031936 or+255768550136 TOVUTI:www.sitenewztanzania,blogspot.com
Na mwandishi wetu magdalena marko
Mpenzi msomaji wa makala ya AFYA YA JAMII
natumai U-mzima wa afya njema na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kla siku
nakusihi ambatana nami katika safu hii ili kujua mambo kadha wa kadha kuhusu
matunda ambapo kwa siku ya leo tutaangalia tunda aina ya chungwa pamoja na
faida zake.
Chungwa ni tunda linalostawi ulimwenguni kote , lakini haswa
tunda hili lilianza kusini mwa bara la Asia, huku likilimwa sana huko nchini
China.
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina
kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe
chungwa lenyewe au juisi yake halisi
Inasadikika kuwa Chungwa
lina kiwango cha juu cha vitamin C, huku nyama /ngozi nyeupe iliyozunguka kati
ya ngozi ya nje na tunda lililomenywa ni chanzo kizuri cha madini ya ‘calcium.’
Endapo unasumbuliwa
na magonjwa magonjwa mbalimbali pamoja na mafua waweza kuongeza maji ya
moto katika juisi ya chungwa kisha kuyanywa.
Majani ya
mchungwa yakipondwa na kisha kuchanganywa na maji ya moto pamoja na asali
kidogo, kwa ujumla mchanganyiko huo hutumika kama dawa ya kikohozi.
Kama maua makavu ya mchungwa yakisagwa
nakuchanganywa katika maji ya moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya
fahamu.
Huku maganda yake
yakisuguliwa usoni huwa ni dawa ya chunusi. Pamoja na hayo, kwa ujumla juisi ya
machungwa husaidia ugonjwa wa pumu, matatizo ya kifua, kusafisha damu, kupooza,
kuungua, matatizo ya meno pamoja na beriberi.
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na
‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la
damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa
presha.
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6
na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli
nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini,
hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa Chungwa moja
lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku.
Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya
kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha
uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili.
Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara,
yakiwemo malaria.
Mbali na magonjwa
hayo, pia husaidia matatizo ya kizazi,mishipa ya damu, magonjwa ya ngozi,
matatizo ya mirija ya uzazi husaidia usagaji wa chakula mwilini pamoja na
kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito
Ifahamike Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa
hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi
yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na
kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata
faida hizo.
Hizo ndizo baadhi ya
dondoo muhumu za faida za machungwa kwa afya ya mwili wako.
Usikose kuungana nami katika mfululizo wa makala ya AFYA YA JAMII ili kufahamu mambo mbalimbali kuhusu matunda
Post a Comment