Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amefuta ziara yake ya kuenda nchini Marekani wiki ijayo kukutana na rais Donald Trump.
Hatua hii inakuja siku moja baada ya bwana Trump kutangaza mpango wake wa kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.
Trump pia alisisitiza kuwa kuwa gharama ya ujenzi wa ukuta huo italipwa na Mexico ambayo tayari imepinga vikali.
Wabunge wa Senate wanasema kuwa bungea la Marekani litaendelea na mpango huo ambao ukadiriwa kuwa utagharimu dola bilioni 12.
Post a Comment