aafisa wa usalama nchini Bangladeshi wametumia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwatambua watatu kati ya magaidi 6 walioshambulia mji mkuu wa Dhaka.
Polisi wanaochunguza shambulizi hilo baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo wanasema Facebook imewasaidia sana.
Afisa hao wa polisi wametangaza hayo huku nchi hiyo ikianza siku mbili za maombolezo.
Ingawa kundi la wapiganaji la Islamic State limesema lilitekeleza shambulio hilo, ambalo lilimalizika baada ya makamando walipovamia jengo la mkahawa jana asubuhi.
Waziri mmoja amesema watu hao walikuwa kwenye kundi la Mujahdeen Bangladesh wala sio Islamic State.
Watu 20 waliuwawa, wengi wao wageni, pamoja na askari polisi wawili.
Wakuu wanasema washambuliaji wote walikuwa waBangladeshi, na walikuwa wakisakwa na maafisa wa usalama
Wapiganaji sita waliuwawa na mmoja alikamatwa.
Post a Comment