0
Wanawake na wazazi wachanga kwa jumla nchini India wanakila sababu ya kutabasamu, baada ya baraza la mawaziri la India Rajya Sabha kuidhinisha mswada unaowapa wanawake likizo ya uzazi ya miezi 6 unusu.
Baraza hilo likiongozwa na waziri mkuu Narendra Modi, liliidhinisha mswada wa mafao ya wazazi wachanga ''The maternity Benefit (Amendment) Bill, 2016, inayoongeza muda wa likizo ya uzazi kutoka majuma 12 hadi 26.
Mabadiliko hayo yanaimarisha sheria ya mwaka wa 1961,iliyoruhusu likizo ya miezi mitatu.
Sheria hii mpya imepigiwa upatu kuimarisha hadhi ya wanawake kazini mbali na kuwasaidia wanawake wenye tajriba ya kazi kusalia makazini mwao hata baada ya kuolewa.
Sheria hiyo mpya pia inawaruhusu wanawake walioasili watoto na hata wale waliosaidiwa kubeba ujauzito kupitia njia ya kisasa ya surrogacy kufaidi likizo hiyo ndefu.
Eneo maalum ya watoto
Image captionMashirika yanayowaajiri zaidi ya wafanya kazi 50 sasa hayatakuwa na budi ila kutenga nafasi maalum ya watoto
Mashirika yanayowaajiri zaidi ya wafanya kazi 50 sasa hayatakuwa na budi ila kuwatengea nafasi maalum ya wazazi kuwanyonyesha watoto wao.
Hatua hiyo imefuatia uchunguzi uliofanywa na mashirika ya kijamii ambao ulionesha kuwa asilimia 50 ya wafanyakazi wanawake huacha kazi punde baada ya kujifungua kwa sababu wanaamini kuwa ni jukumu la wanawake kuwalea watoto wao wala sio jukumu la wazazi wote wawili.
Likizo ya uzazi India ni miezi 6!
Image captionLikizo ya uzazi India ni miezi 6!
India imeorodheshwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya wanawake walioajiriwa, jambo ambalo serikali inajaribu kubadilisha.

Post a Comment

 
Top