Mawakili wa FIFA wasema washukiwa wakuu wa madai ya ufisadi ambao hadi hivi majuzi walikuwa wakiliongoza shirikisho hilo la kandanda duniani walijilimbikizia nyongeza za mishahara na marupurupu mengineyo ambayo yamejumuishwa na kufika dola millioni 80.
FIFA imeelezea kuwa malipo hayo yaliodhinishwa katika kipindi cha miaka mitano na kupewa miongoni mwao Sepp Blatter, Jerome Valcke na Markus Kattner si halali kwa mujibu wa sheria za Uswizi.
Ushahidi unaokusanywa utakabidhiwa waendesha mashtaka wa Marekani na Uswizi
FIFA imeyafichua hayo baada ya polisi wa Uswizi kufanya uvamizi katika ofisi zilizoko makao makuu ya Zurich nchini Uswizi.
Tayari akina Blatter na Valcke wameshafunguliwa mashtaka mengine ya matumizi mabaya ya fedha za FIFA madai wanayokana.
Post a Comment