0
Mvulana mwenye umri wa miaka saba,Yamato Tanooka aliyepotea nchini Japan Jumamosi iliyopita sasa amepatikana akiwa hai.
Maafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.
Image copyrightAFP
Image captionYamato Tanooka 7,aliyekuwa amepotea nchini Japan
Kijana huyo huyo ambaye aliachwa na babake mwituni kama adhabu alitembea kwa zaidi ya kilomita 4 hadi ukingoni wa msitu huo alipotulia.
Anasemekana kuwa katika hali nzuri ya kiafya ingawa amepelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Image copyrightAP
Image captionMaafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.
Inasemekana kuwa alipopatikana alikuwa na njaa na baridi lakini katika hali nzuri.
Babake mtoto huyo aliwambia waandishi wa habari kuwa alimwomba msamaha na kuwa alifurahi kuwa mwanawe alipatikana akiwa hai.

Post a Comment

 
Top