0
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, amemteua binti yake kuwa mkuu wa shirika la mafuta la kitaifa la Sonagol.

Image captionIsabel dos Santos ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika

Rais aliwaachisha kazi wanachama wote wa bodi ya shirika hilo mnamo mwezi Aprili, mwaka huu.
Vyombo vya habari nchini vinasema kuwa Isabel dos Santos anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika shirika hilo ili kuimarisha utendakazi na faida katika shirika hilo.

Image copyrightAFP
Image captionAngola ni taifa la pili katika uzalishaji wa mafuta barani la Afrika.

Angola ni taifa la pili katika uzalishaji wa mafuta barani la Afrika.
Binti dos Santos ambaye ametambuliwa na jarida la Forbes kama mwanamke tajiri zaidi barani Afrika; tayari ameekeza katika sekta ya simiti, benki na mashirika ya mawasiliano na uchimbaji wa almasi.

Post a Comment

 
Top