Serikali ya Mexico imewataka raia wake wanaoishi Marekani kuchukua tahadhari zaidi mbali na kuwasiliana kwa karibu na ubalozi wao kutokana na kauli za utawala mpya wa Bw. Trump kwamba watafurushwa kutoka Marekani.
Kauli hiyo inakuja baada ya kufurushwa kutoka Marekani kwa mwanamke mmoja raia wa Mexico Guadalupe Garcia de Rayos hapo juzi .
- Trump: Mexico watalipia ukuta '100%'
- Rais wa Mexico afuta ziara yake Marekani
- Mexico: Hatutalipia ukuta wa Donald Trump
- Trump kuzuru Mexico licha ya msimamo mkali
Bi Guadalupe Garcia alikuwa amekwendwa kwa huduma za kawaida katika ofisi ya uhamiaji ya Marekani lakini badala yake akafurushwa kutoka nchini humo.
Sasa serikali ya Mexico inasema hii ni dhahiri kuwa raia wake watakabiliwa na masharti magumu ya kuingia na kuishi Marekani - hivyo kuwashauri wawe na mpango wa dharura ili kuwasaidia iwapo itawalazimu kuihama Marekani kwa haraka .
Post a Comment