0
BODI ya Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), imeitaka serikali kupitisha Sheria ya Majengo ili kuwabana wataalamu wa ujenzi watakaokwenda kinyume na taratibu.
Pia amewataka watanzania kuwatumia wataalamu wa majenzi pindi wanapotaka kujenga ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza kutokana na ujenzi usiozingatia taratibu.
Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa alisema uwepo wa Sheria ya Majengo utawezesha kuwabana wataalamu wa fani hiyo pale watakapokwenda kinyume na taratibu za ujenzi.
Alisema kwa sasa fani hiyo ina wataalamu 1,400 na kwamba kati yao waliobobea katika fani ni 800 pekee.
“Sheria hii itasaidia kupunguza ajali za majengo zinazochangiwa na wataalamu wasio na viwango,” alisema Mwakyusa.
Kaimu Msajili ambaye pia ni mkadiriaji majenzi, Mashaka Bundala alishukuru uwepo wa maonesho hayo ambayo yamekutanisha wataalamu wa fani mbalimbali na kubadilishana uzoefu.

Post a Comment

 
Top