0
Arsene Wenger amemwambia Ian Wright kwamba muda wake kama mkufunzi wa Arsenla unakaribia kikomo kulingana na mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.
Wenger ameifunza Arsenal tangu mwezi Oktoba 1996 na mara ya mwisho yeye kushinda taji la ligi ilikuwa mwaka 2004.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu huu.
''Ninahisi kwamba ameamua'', mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal aliambia BBC Radio 5 live.
''Anaonekana amechoka.Unahisi kwamba anaonyesha uchovu.Nadhani atawachia mwishoni mwa msimu huu''.
Matumaini ya Arsenal ya kushinda taji la ligi msimu huu yalipata pigo kubwa baada ya kushindwa 3-1 na viongozi wa ligi Chelsea kuwawacha wakiwa pointi 12 nyuma ya ChelseaWright anasema kuwa aliongea na Wenger usiku wa Alhamisi.
''Aliniambia kwamba anafikia kikomo.Sijamsikia akisema hivyo awali'',alisema Ian Wright mwenye umri wa miaka 53.
''Wachezaji wamemuangusha sana.Iwapo hataondoka mwisho wa msimu huu kutakuwa na mabadiliko makubwa mwishoni mwa msimu huu.Wanafaa kujiangalia sana.Amekuwa mwaminifu kwa timu hii''.
Baadhi ya mashabiki wamemtaka Wenger kuondoka ,huku mmoja akibeba bango katika uwanja wa Stamford Bridge lililosema ''Imetosha! Ni wakati unafaa kuondoka''..

Post a Comment

 
Top