Donald Trump anasema kuwa huenda akabadilisha marufuku yake dhidi ya wahamiaji na agizo jingine la rais litakalopiga marufuku raia wa mataifa kadhaa kutoingia Marekani baada ya jaribio lake la awali kubadilishwa na mahakama.
Bw Trump aliambia wanahabari katika ndege ya Airfoce One kwamba amri mpya huenda ikatolewa mapema siku ya Jumatatu ama jumanne .Inajiri baada ya mahakama ya rufaa mjini San Fransisco kupinga amri yake ya hapo awali.
Agizo hilo lilikuwa limepiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Waislamu.
Haijulikani ni vipi amri hiyo mpya itakuwa.
Bw Trump amesema kuwa amri hiyo itakuwa na mabadilik kidogo lakini hakutoa maelezo zaidi.
Post a Comment