0
Kampuni inayofanya vizuri Afrika katika suluhisho za malipo ya mitandaoni na ya kupitia mitandao ya simu, 3G Direct Pay leo imezindua suluhisho jipya la programu ya simu (mobile app) ambayo itawawezesha kufanya biashara za malipo ya kadi na simu kupitia simu zao mahali popote na kwa wakati wowote.
Programu hiyo inayoitwa mSWIPE+ inawezesha wafanyabiashara kuhakiki malipo kupitia simu zao na pia kuweza kusoma kadi za malipo yanayopitia katika mashine za mauzo (POS) kupitia mfumo unaoitwa Quickpay. Programu hii ya mSwipe+ inaweza kutumika kwa aina zote za kadi za malipo ya kabla na baada (credit na debit cards) na pia malipo ya kutumia simu za mkononi.
Mkurugenzi Mkuu wa 3G Direct Pay, Eran Feinstein, amesema kuwa programu hiyo imeundwa kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara na wateja wao, kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahali popote na pia kuboresha maendeleo ya malipo ya kadi na biashara za mitandaoni.
“Simu ya mkononi ni muhimu sana katika maisha ya watu wengi. Na programu hii inawezesha malipo kufanyika kupitia huu mtandao. Na hii ni katika mipango yetu ya kuhakikisha kuwa mtu yeyote ana uhuru wa kununua, kuuza, kulipa na kulipwa kupitia mtandaoni kwa haraka, usalama na urahisi. Programu ya mSwipe+ ni njia rahisi, ya haraka na yenye usalama inayompa mteja uhuru wa kutumia kadi ya aina yoyote ya malipo, malipo ya kupitia simu, na kuweza kulipa mara moja,” alioongeza Feinstein.
Programu ya mSWIPE+ kwa sasa inatumika tu kwenye simu za teknolojia ya android na inaweza kutumika tu kwa wale wafanyabiashara watakaojisajili na mtandao wa 3G Direct Pay na programu hiyo inapatikana katika simu kwenye ‘Google Play Store’ Kwa simu zinazotumia teknolojia ya IOS bado ujenzi wa programu yao unaendelea.
Programu ya mSwipe+ ina teknolojia ya ulinzi na usalama wa kimtandao wa kuhakikisha malipo yoyote yanayofanyika ni salama kwa watumiaji.

Post a Comment

 
Top