Bingwa mara tano tenis kwa upande wa wanawake Venus Williams dada yake Serena Williams amemchapa mkazakhatan Yaroslava Shvedova na hivyo kuingia nusu fainali ya Wembledon kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.
Na sasa kuna uwezekano mkubwa Venus atakutana na mdogo wake, Serena Williams ambaye amemchapa Mrusi Anastasia Pavlyuchenkova.
Kwa hivyo sasa wawili hawa wote wameingia nusu fainali ambapo kesho alhamis Serena atacheza na mrusi Elena Vesnina naye Venus atapambana na Mjerumani Angelique Kerber.
Sasa iwapo Serena atamshinda Elena na Venus akamshinda Angelique basi Fainali itakuwa kati ya mabinti hawa wawili wa Mzee Wiliiams.
Post a Comment