0


Rais wa Marekani Donald Trump amemkaribisha waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, kusafiri nae katika ndege yake Air Force One wakielekea Florida wikiendi hii ambako wataendelea na mazungumzo yao huku wakicheza gofu.
Awali katika ikulu ya White house, Trump amemhakikishia kiongozi huyo kuhusu kuendelea kusaidia kudumisha usalama wa Japan na kwamba uhusiano wao ni nguzo muhimu kwa amani na utulivu wa eneo la Asia Pacific..
Alipozungumza huko ikulu ya White House, waziri mkuu Abe amesema pia wamekubaliana kulipa kipua mbele swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia vinavyotolewa na Korea Kazkazini..
Bw Trump ametoa hakikisho kwamba majadiliano ya kibiashara baina ya Marekani na Japan yatakuwa ya uwiano mzuri wa kufaidi mataifa yote mawili.
Bw Abe kwa upande wake amesema kuwa mazungumzo yao ya baadae leo yatalenga kuchambua zaidi mkataba wa kibiashara wa Trans-Pacific ambao Trump amekuwa akisema Marekani haina nia ya kuuendeleza .

Post a Comment

 
Top