0
Shirika la Amnesty International limedai serikali ya Sudan imekuwa ikitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake eneo la Darfur, na kwamba watoto 200 ni miongoni mwa waliofariki.
Vifo hivyo vinadaiwa kutokea kuanzia Januari mwaka huu.
Wale wanaoathiriwa na "moshi wenye sumu" kutoka kwa silaha hizo hutapika damu, kupata matatizo ya kupumua na ngozi zao huchubuka.
Serikali ya Sudan imekuwa ikikabiliana na waasi kwa miaka 13 Darfur.
Hata hivyo, madhila ya raia hayajakuwa yakiangaziwa sana tangu 2004 pale wasiwasi wa kutokea kwa mauaji ya halaiki ulipoifanya jamii ya kimataifa kuchukua hatua.
Sasa, ripoti mpya ya Amnesty International inasema mashambulio ambayo yamekuwa yakitekelezwa na serikali ya Sudan dhidi ya raia wake yanaonesha hakuna chochote kilichobadilika, kwa mujibu wa Tirana Hassan, mkurugenzi wa utafiti wa Amnesty maeneo ya mizozo.
Shirika hilo la kutetea haki za kibinadamu linasema uchunguzi wa miezi minane umefichua serikali ilitumia mbinu za kuteketeza kila kitu, kubaka watu, kuua na kurusha mabomu eneo la Jebel Marra, Darfur.
Watafiti walipata watu 56 wanaosema walishuhudiwa silaha za kemikali zikitumiwa zaidi ya mara 30 na wanajeshi wa Sudan ambao walianza operesheni ya kijeshi dhidi ya waasi wa Sudan Liberation Army, wanaaongozwa na Abdul Wahid (SLA/AW) katikati mwa Januari.
"Ni vigumu kueleza ukatili uliotekelezwa," anasema Bi Hassan. Picha na video tulizoona wakati wa uchunguzi huu zinaogofya. Katika moja, mtoto analia kwa uchungu kabla ya kufariki. Picha nyingi zinaonesha watoto wakiwa na vidonda kwenye ngozi. Wengine hawangeweza kupumua na wengine wanatapika damu."
Mkono wa mtoto ukionyesha vidonda ambavyo ni sawa na vinavyosababishwa na silaha za kemikaliImage copyrightAMNESTY INTERNATIONAL
Image captionMkono wa mtoto ukionyesha vidonda ambavyo ni sawa na vinavyosababishwa na silaha za kemikali
Manusura waliambia Amnesty International kwamba moshi wa harufu isiyo ya kawaida ulitanda angani baada ya mabomu kurushwa.
Ramani ikionyesha eneo la Jebel Marra, Sudan
Image captionJebel Marra ni moja ya maeneo yenye rotuba zaidi Darfur
Amnesty wamesema wametuma nakala ya ripoti hiyo kwa serikali ya Sudan lakini bado hawajapokea jawabu.

Post a Comment

 
Top