0
Waumini 30 wa dini ya kiislamu wamekufa maji Kaskazini mwa Pakistan baada ya mafuriko ya ghafla kukumba eneo hilo na kusomba msikiti wao .
Halmashauri ya kukabiliana na majanga nchini humo inasema kuwa hakuna aliyesalia hai katika msikikiti huo wa Ursoonulioko katika wilaya ya Chitral.
Image copyrightAFP
Image captionMafuriko katika eno hilo mwaka uliopita yalisababisha vifo vya watu kadha
Waumini hao waliokuwa wakiswali na kusikiza maubiri ya usiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhan walipatwa ghafla na wimbi kubwa la maji.
Vyombo vya dola vya utabiri wa hali ya anga vinasema hii ndio mara ya kwanza kabisa kwa mafuriko makubwa na yenye kina kirefu zaidi kuwaikukumba eneo hilo la Kaskazini mwa Pakistan.
Eneo hilo lipo kimo cha takriban mita 8,000 juu ya usawa wa bahari.
Image copyrightAP
Image captionEneo hilo lipo kimo cha takriban mita 8,000 juu ya usawa wa bahari.
Maafisa wanane wa usalama waliokwenda kuwanusuru wahanga wa mafuriko hayo nao hawajulikani waliko baada ya kituo chao kusombwa na mafuriko.
Mafuriko katika eno hilo mwaka uliopita yalisababisha vifo vya watu kadha na kuharibu madaraja.

Post a Comment

 
Top