0
Mwenyekiti ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amejiuzulu miezi miwili tu baada ya kushika usukani.
Alichukua nafasi hiyo kama mwenyekiti wa kampeni, baada ya meneja wa zamani Corey Lewandowski kufutwa kazi mwezi Juni.
Mtaalamu huyo wa masuala ya siasa wa umri wa miaka 67, amekuwa chini ya shinikizo kufuatia uhusiano wake na rais wa zamani wa Ukrain Viktor Yanukovych ambaye anaipendelea Urusi.
Lakini haijulikani ni kwa nini aliondoka kutoka kwa kundi hilo la kampeni lililofanyiwa mabadiliko wiki hii kwa kuongezwa meneja mpya pamoja na mkurugeni mkuu.
Bwana Manafort amekosolewa siku za hivi karibuni baada ya gazeti la New York times kuripoti kuwa serikali ya Ukrain ilifichua ahadi za kumlipa dola milioni 12 kwa kumfanyia kazi bwana Yanukovych.

Post a Comment

 
Top