0
Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la kubebea wagonjwa Syria, imeweka wazi tena madhila wanayopitia raia nchini Syria.
Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.
Picha hiyo ya Omran, 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana katika ufukwe wa Uturuki mwaka jana.
Omran alitolewa kwenye vifusi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la kutoka angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.
Jamii ya kimataifa imeguswa na wito wa kusitishwa kwa mapigano kutolewa.
Mshirika mkuu wa Rais Bashar al-Assad, Urusi, imesema iko tayari kusitisha vita katika mji huo wa kaskazini kwa saa 48 kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
"Nimepiga picha nyingi za watoto waliouawa au kujeruhiwa wakati wa mashambulio yanayotekelezwa kila siku," mpiga picha hiyo Mahmoud Rslan aliambia AFP.
"Kawaida, huwa wamepoteza fahamu au wanalia. Lakini Omran alikuwa amekaa hapo, bila kutamka neno, akionekana kuduwaa, kana kwamba hakuwa anafahamu nini kilichokuwa kimetokea."
Mwili wa Ayran Kurdi ukiondolewa kwenye ufukwe wa bahari Uturuki mwaka janaImage copyrightAYRAN KURDI
Image captionMwili wa Ayran Kurdi ukiondolewa kwenye ufukwe wa bahari Uturuki mwaka jana
Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini Syria.
Zaidi ya watu 17,700 wanakadiriwa kufariki wakiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.

Post a Comment

 
Top