Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza Mauricio Pochettino amemelezea kiungo wa kati wa klabu hiyo kutoka Kenya Victor Wanyama kama "mnyama".
Amesema mchezaji huyo ana sifa, nguvu na uwezo wa kuifaa sana klabu hiyo msimu huu.
"Ni mnyama, ninamfahamu vyema kwa sababu nilimnunua nikiwa Southampton kutoka Celtic. Ni rahisi sana kutambua sifa hizi," alisema.
Meneja huyo alikuwa anajibu maswali kuhusu umuhimu wa mchezaji huyo kwa klabu hiyo kwenye kikao na wanahabari katika kituo cha mafunzo cha klabu hiyo London.
Pochettino, raia wa Argentina, alijiunga na Spurs Mei 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na Mei mwaka huu aliongeza mkataba huo na kuahidi kusalia White Hart Lane hadi 2021.
Wanyama alinunuliwa £11m na Spurs kutoka Southampton mwezi Juni mwaka huu na kujiunga na Ponchettino, meneja aliyemnunua kutoka Celtic kwa £12.5m mwaka 2013.
Kabla ya kuhamia Celtic, Mkenya huyo alikuwa anachezea Germinal Beerschot ya Ubelgiji.
Post a Comment