Arsenal wamekubali kumsajili mshambulizi chipukizi kutoka Japan Takuma Asano.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 21 amejiunga na the Gunners akitokea klabu ya nyumbani ya Sanfrecce Hiroshima.
Kandarasi yake hata hivyo itakamilishwa baada ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Arsenal imechapisha kwenye tovuti yake picha za mashambulizi huyo na kumkaribisha uwanjani emirati.
Takuma amewahi kuichezea Japan katika mechi 5 za kimataifa.
Takuma anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakayoshiriki michezo ya Olimpiki mwezi ujao jijini Rio de Janeiro Brazil.
Takuma amecheza mechi 56 na kufunga mabao 11 katika ligi kuu ya Japan J-League.
Alishinda ligi hiyo ya J1 League mwaka wa 2013 na 2015, Japanese Super Cup 2013, 2014 na 2015,mwaka huo pia alituzwa kama chipukizi bora wa mwaka .
Kocha Arsène Wenger amemsifu mshambulizi huyo kwa ukakamavu wake
''Takuma ni mshambulizi machachari sana na bila shaka atatufaa zaidi katika siku za usoni.Bila shaka ameanza vyema taaluma yake na tunatazamia kukinoa zaidi kipaji chake kwa manufaa ya Arsenal''.
Post a Comment