0
Uingereza imezuia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya ambapo itakuwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwa miaka 40.
Waziri Mkuu, David Cameron, hatakuwa mezani wakati viongozi wengine 27 wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya watakuwa wakihudhuria mkutano usio rasmi juu ya hatma ya muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza.
Uingereza imeambiwa ianzishe mpango wake wa kuondoka katika jumuiya hiyo bila kuchelewa.
Rais wa Jumuiya ya Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa shughuli za kutegua kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano huo zinapaswa kutekelezwa mara tu Uingereza inapompata Waziri Mkuu mpya.

Post a Comment

 
Top