0
Vyombo vya Habari nchini Ethiopia vimeripoti kuwa watu kadhaa wameuawa katika maandamano yenye vurugu yaliyofanyika kaskazini mwa nchi hiyo.
Ghasia hizo zilisambaa pia jana katika mji wa Sirinka, ambao ni wa nne kukumbwa na ghasia hizo.
Barabara zinaelezwa kuwa ziliwekwa vizuizi na majengo ya serikali kushambulia.
Maandamano hayo yalianza wiki iliyopita baada ya majeshi ya serikali kushambulia waumini wakati wa sherehe za kidini katika mji wa Weldiya, na kusababisha vifo vya watu watano.
Uamuzi wa hivi karibuni wa serikali kuwaachia huru maelfu ya wanaharakati haukutuliza maandamanao hayo, ambayo yamekuwa yakifanyika karibu miaka mitatu sasa.

Post a Comment

 
Top