Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amefuta ziara yake nchini Algeria kufuatia kile kinachotajwa kuwa afya mbaya ya rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika.
Rais Bouteflika wa umri wa miaka 79 anasumbuliwa na tatizo la kupumua kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya rais iliyochopishwa na shirika la APS.
Bi Merkel anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Bouteflika katika masuala ya usalama na uhamiaji.
Sasa ziara hiyo itapangwa siku tafauti, kwa mujibu wa ofisi ya rais.
Bwana Boutfkliua, alipatwa aa kiharusi mwaka 2013 na si rahisi kuonekana hadharani.
Post a Comment