0
Maafisa wa polisi wa kutuliza ghasia nchini Marekani, wamewaondoa maelfu ya waandamanaji walioshiriki katika maandamano makubwa nje ya eneo la mkutano wa chama cha Republican, ambapo mgombea wa tiketi ya urais wa chama hicho Donald Trump alikuwa akihutubia.
Mgombea huyo aliingia katika eneo la mkutano chini ya ulinzi wa maafisa wanaomlinda rais wa Marekani maarufu kama Secret service, kupitia mlango wa nyuma.
Image copyrightReuters
Image captionMaandamano katika mkutano wa Trump
Bwana Trump amewaambia wajumbe wa chama hicho kuwa wanafaa kumuunga mkono kwani kinyanganyiro cha wagombea wa Republican kimefikia kikomo.
Waandamanaji wamekuwa wakisambaratisha mikutano ya Donald Trump katika maeneo tofauti nchini Marekani, kutokana na msimamo wake dhidi ya waislamu na wahamiaji.

Post a Comment

 
Top