0
Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki umewasili leo alfajiri mjini Nairobi ukitokea London Uingereza na kutumbukiza taifa zima katika kipindi cha maombolezi.
Mabaki ya bi Kibaki yalilakiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na rais Uhuru Kenyatta Naibu wake William Ruto na viongozi na wakenya wa haiba mbalimbali mwendo wa saa kumi na moja .
Ndege iliyoileta familia ya rais Kibaki ilitua saa kumi na moja na dakika tatu na kupewa hadhi ya kitaifa.
Image captionMwili wa Lucy Kibaki wawasili Kenya
Kwaya aliyoipenda wakati wa maisha yake ya Mama Lucy ndio iliyowaongoa waombolezaji wakati jeneza lake lililofunikwa na bendera ya taifa ilipotolewa kwenye ndege hiyo ya Kenya Airways na wanajeshi wa jeshi la Kenya.
Huzuni ilighubika umati wa viongozi waliofika uwanjani kuulaki mwili wake.
Image captionRais Uhuru Kenyatta akimliwaza mtangulizi wake rais Mwai Kibaki
Machozi yaliwalengalenga huku baadhi yao walioshindwa kustahimili waliangua kilio.
Jeneza hilo liliwekwa kwenye hema ndogo kabla ya kasisi Dominic Wamugunda kuongoza misa fupi ya wafu.
Image captionJeneza hilo liliwekwa kwenye hema ndogo kabla ya kasisi Dominic Wamugunda kuongoza misa fupi ya wafu.
Kisha mwili huo ukapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ya Lee Funeral.
Msemaji wa serikali bwana Eric Kiraithe amesema kuwa tarehe kamili ya mazishi itatangazwa baadaye kutokana na itifaki baada ya serikali kuamua kumpa mazishi ya kitaifa.
Image captionKasisi Dominic Wamugunda akiongoza misa fupi ya wafu katika angatua ya Jomo Kenyatta
Hata hivyo vitabu vya risala za rambirambi vitafunguliwa katika kanisa la Holy Family Basilica, na Consolata Shrine pamoja na afisi za serikali kote nchini.
Mama Lucy, 82 aliaga dunia jumanne iliyopita katika hospitali ya Bupa Cromwell iliyoko London Uingereza alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya ziada.
Image captionMama Lucy, 82 aliaga dunia Jumanne iliyopita katika hospitali ya Bupa Cromwell iliyoko London
Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka akiwaamekasirishwa na jinsi habari moja ilivyoandikwa.
Image captionMsemaji wa serikali bwana Eric Kiraithe amesema kuwa tarehe kamili ya mazishi itatangazwa baadaye kutokana na itifaki
Katika kumbukumbu ya kumhenzi bi Kibaki rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alimsifu kwa jukumu lake kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya.
Bw Kenyatta alimrithi mumewe bw Kibaki ambaye alitawala kati ya mwaka 2002- 2013.
Rais Kenyatta alitangaza kuanza rasmi kwa siku tatu za maombolezi alipochapisha picha hizi kwenye mtandao wake wa Facebook.
Aidha alitangaza bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti katika muda huu wa maombolezi.

Post a Comment

 
Top