0
Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya zoezi la ushirikiano la kukabiliana na makombora katika maji ya jimbo la Hawaii.
Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa majiribio ya makombora ya masafa mafupi katika miezi ya hivi karibuni inayofanywa na Korea kaskazini.
Image captionManuari ya kijeshi
Majaribio mengi hatahivyo hayakufanikiwa lakini ufanisi wa kombora la sita hivi majuzi ulilishangaza eneo hilo.
Korea Kaskazini ambayo imefanya majaribio manne ya mokombora ya kinuklia imesema kuwa zoezi hilo ni la uchokozi wa kijeshi.
Image copyrightGETTY
Image captionZoezi la kijeshi
Vyombo vya habari vimesema kuwa Marekani pamoja na vikosi vyengine ni tishio la mara kwa mara la usalama wa Korea Kaskazini na hivyobasi kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na makombora ya masafa marefu na yale ya kinuklia.

Post a Comment

 
Top