0
Liverpool wamekamilisha shughuli ya kumsajili Sadio Mane kwa kima cha dola milioni 45 kutoka Southampton.
Wachambuzi wa michezo sasa wanasema kuwa hatua hiyo inasababisha yeye kuwa mcheza soka ghali zaidi barani Afrika.
Mane raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 21 katika mechi 67 za ligi kuu kwa Southmpton, baada ya kijiunga nao kwa dola milioni 13 kutoka Salzburg mwaka 2014.
Amesema amefurahishwa zaidi kwa kujiunga na moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya.

Post a Comment

 
Top