0
Wanaume walio na viuno vikubwa wako hatarini kupatikana na saratani ya tezi dume ,utafiti umebaini.
Utafiti uliofanyiwa watu 140,000 kutoka mataifa manane ya Ulaya ulibaini kwamba viuno vikubwa huongeza mtu kupatikana na saratani hiyo kwa asilimia 13.
Wanaume ndio waliomo hatarini zaidi wakiwa na ukubwa wa nchi 37 ,kulingana na utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford.
Saratani ya tezi dume ndio ilio na visa vingi miongoni mwa wanaume.
Utafiti huo uliowasilishwa katika mkutano wa ugonjwa wa kunenepa uliofanyika mjini Gothenburg nchini Sweden uliangazia ushirikiano wa vipimo vya mwili miongoni mwa wanaume walio katika umri wa miaka 50 na hatari za saratani ya tewzi dume katika kipindi cha miaka 14.
Katika wakati huo kulikuwa na visa 7000 vya saratani ya tezi dume huku watu 934 waliokuwa na ugonjwa huo wakifariki.
Utafiti huo ulibaini kwamba wanaume walio na miili pamoja na viuno vikubwa walikuwa na hatari ya kupatikana na ugonjwa huo.

Post a Comment

 
Top