Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa nyara kwake na kundi la wanamgambo wa Al Qaeda.
Katika mahojiano na BBC, Ali Haider Gilani amesema Al Qaeda walimwambia kuwa kutekwa kwake ni hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya Baba yake.
Watekaji walitaka kulipwa pesa na kuachiwa kwa wafungwa wa kundi la wanamgambo hao.
Gilani aliokolewa kutokana na Operesheni inayofanywa na Marekani na Afghanistan katika jimbo la Paktika
Post a Comment