Mapigano katika mji wa bandari wa Aden, Yemen, yanaarifiwa kutulia kwa sasa baada ya kutokea ghasia kati ya wapinzani wa muda mrefu, katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Watu kadhaa wakiwemo raia wameuawa ama kujeruhiwa katika mapigano kati ya wapiganaji wanaotaa kujitenga na kupata uhuru wao, Yemen ya Kusini, na majeshi ya serikali ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Saudi Arabia.
Wote kwa pamoja serikali ambayo imepiga kambi kwa muda katika mji wa Aden na viongozi wa kundi linalotaka kujitenga wameyaagiza majeshi yao kusimamisha mapigano na kuwataka washirika wao wa Kiarabu kujaribu kutuliza hali.
Mapigano ya pande hizo mbili yamekuwa yakizidisha hali mbaya ya kibinadamu iliyosababishwa na mzozo na waasi wa Ki houthi kwa muda sasa
Post a Comment