Wanaume wanne wamefikishwa kwenye
mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu,
baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema
kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
- Mgahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''
- Hoteli yafungwa kwa madai ya kuuza nyama ya ng'ombe India
- Sherehe ya kula nyama ya mbwa yafanyika China
- Mjenga misuli ala kondo la nyuma la mpenziwe
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.
Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari ya kitamadunia.
Post a Comment