Si jambo linaloweza kufikiriwa na kila mtu kulitenda wakati wa siku maalum, Lakini wapenzi wa kichina walichagua kusherehekea harusi yao huku wakielea angani katika daraja la kioo.
Bibi harusi na bwana harusi walioana katika daraja la Shiniuzhai katika mji wa Pingjiang jimbo la Hunan katika siku ya wapendanao ya uchina inayoadhimishwa tarehe 9 Agosti, Shirika la habari la China News Service limeripoti.
Licha ya kuelea angani yapata futi 590 kutoka usawa wa ardhi , waliweza kuonyesha tabasamu zao walipokuwa wakipigwa picha za harusi yao.
Madaraja ya vioo yamekuwa maarufu sana nchini uchina hivi karibuni.
Wiki chache tu zilizopita , maharusi wengine waliamua kuvalishana pete kwenye daraja hilo hili ingawa hawakutoka kwenye daraja
Post a Comment