0
Raia nchini Iran wanapiga kura katika awamu ya pili ya uchaguzi utakaoamua ugavi wa mamlaka kati ya mrengo wa wastani na wahafidhina katika bunge la nchi hiyo. Katika awamu ya kwanza Februari, wafuasi wanaopendelea mageuzi walishinda kwa kiasi kizuri lakini wanahitaji kushinda viti 40 zaidi kudhibiti bunge lenye viti 290.
Uchaguzi Ijumaa unafanyika katika majimbo 68 ambapo hakuna mgombea aliyeshinda kima kinachohitajika cha 25% ya kura hiyo.
Matokeo yanatarajiwa Jumapili.
Kura ya Februari ni ya kwanza kufanyika tangu Iran itie saini makubaliano ya nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani na imeonekana kama mtihani kwa rais Hassan Rouhani anayependa mageuzi.
Image copyrightAP
Image captionRais Hassan Rouhani
Washirika wa mrengo wa wastani wa rais Rouhani walishinda viti 106 kwa ushinidi mkubwa kwenye mji mkuu, Tehran.
Matokeo ya Tehran ni muhimu kwa sababu wabunge kutoka mjihuo kwa mara nyingi hudhihirisha muelekeo wa bunge, wachambuzi wanasema.
Wafuasi wanaopendelea magezui pia walishinda katika uchaguzi wa bunge la wataalamu, linalomteua kiongozi mwenye nguvu nchini humo, kiongozi mkuu.
Waandishi wanasema licha ya kuwa uchaguzi wa wabunge hautarajiwi kuidhinisha mageuzi makubwa katika sera za nchi hiyo, huenda ukamsaidia rais Rouhani kushinikiza mageuzi ya uchumi na kijamii.

Post a Comment

 
Top