0
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anazidi kufanya maboresho katika msimu wa 2016/2017 ili kuiwezesha timu yake kuibuka na makombe zaidi baada ya msimu uliopita kushindwa kunyakua kombe lolote katika michuano yote iliyoshiriki.
Taarifa ambayo imetoka leo inaeleza kuwa Arsenal imefikia makubaliano na klabu ya Sanfrecce Heroshima ili kumpata mshambuliaji kinda wa klabu hiyo raia wa Japan, Takuma Asano, 21.
Akimzungumzia mchezaji huyo, Wenger alisema kuwa “Takuma ni mchezaji mdogo na mwenye kipaji nadhani atakuwa mzuri zaidi kwa kizazi kijacho”
Pamoja na umri wa miaka 21, kinda huyo wa Japan katika historia yake ya soka amefanikiwa kufunga 20 katika michezo 75 na kushinda kombe la J1 League mara mbili, Japanese Super Cup mara 3, AFC U23 Championship na J League Rookie of the Year 2015.

Post a Comment

 
Top