0
Manchester United wanataka kumsajili mshambulaji wa Ubelgiji Dries Mertens 30. (Calcio Mercato, in Italian)
Kandarasi ya Marouane Fellaini inakamilika mwisho wa msimu huu katika klabu ya Manchester United lakini raia huyo wa Ubelgiji ana matumaini kwamba atatia saini kandarsi mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Daily Mirror)
Image caption Kandarasi ya Marouane Fellaini inakamilika mwisho wa msimu huu katika klabu ya Manchester United
Wakati huohuo, Manchester United wanataka kumsajili mwana wa beki Phil Neville .Harvey Neville anaichezea klabu ya kinda ya Valencia, klabu ambayo babake alikuwa naibu wa kocha 2015. (Super Deporte, in Spanish)
Inter Milan wanamlenga mchezaji anayesakwa na Liverpool Marco Reus, huku kiungo huyo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani , 28, akitarajiwa kurudi mapema mwaka ujao baada ya kuuguza jeraha. (transfermarketweb.com)
Image caption Crystal Palace wanataka kumsajili mchezaji wa Ujerumani aliyezaliwa Uturuki na mshambuliaji wa Besikitas Cenk Tosun
Crystal Palace wanataka kumsajili mchezaji wa Ujerumani aliyezaliwa Uturuki na mshambuliaji wa Besikitas Cenk Tosun, 26, ambaye ana thamani ya Yuro 25m (Croydon Advertiser)
Arsenal inataka kumsajili kiungo wa kati wa Trabzonspor Abdulkadir Omur lakini wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka klabu ya Uhispania Atletico Madrid kwa mchezaji huyo wa miaka 18.(Sun)
Image caption Antonio Conte
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte alibakia amekasirishwa msimu uliopita baada ya klabu hiyo ya Stamford Bridge kushindwa kumnunua mshambuliaji Fernando Liorente ,ambaye baadaye alielekea Tottenham kutoka Swansea kwa kitita cha pauni milioni 11.5 (Times - subscription required)
Winga wa Benfica na Peru Andre Carrillo, 26, anataka kuibadilisha kandarasi yake ya mkopo katika klabu ya Watford kuwa uhamisho wa kudumu baada ya kuonyesha mchezo mzuri . (Watford Observer)

Post a Comment

 
Top