0
Mahakama kuu Afrika kusini imeruhusu kuangaliwa upya uamuzi uliopitishwa 2009 wa kutupilia mbalia mashtaka yote ya ufisadi dhidi ya rais Jacob Zuma.
Majaji wamesema kaimu mkurugenzi wa upande wa mashtaka alichukuwa hatua kwa wepesi ya kuondosha mashtaka takriban 800 dhidi ya Zuma.
Mwendesha mashtaka ametetea uamuzi huo kwa misingi kuwa serikali iliingilia kati kesi hiyo, inayohusu makubaliano ya biashara ya silaha zenye thamani za mabilioni ya dola.
Lakini mahakama kuu imesema upande wa mashtaka unaonekana kuwa ulikuwa tayari kuendelea na kesi hadi usiku wa kuamkia kuwasilishwa tangazo hilo, hatua iliyotoa nafasi kwa Zuma kuwania urais.
Ushahidi umetokana na 'kanda za kijasusi' - ambazo ni mazungumzo ya simu yalionakiliwa kati ya aliyekuwa jasusi wa Afrika ksuini na aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu, ambapo wanasikika wakipanga kumzuia Zuma kuwania urais nchini humo.
kwa miaka mingi upinzaniumetaka upewe kanda hizo- ukidai kuwa ushahidi wa rushwa huedna ukawa pia uko kwenye kanda hizo.
Upinzani kwa mara nyengine umetaka rais Jacob Zuma ajiuzulu,abaye tayari yumo kwenye shinikizo baada ya kupatikana kukiuka katiba kwa kutozingatia matokeo yaliofichuliwa na taasii ya serikali.

Post a Comment

 
Top