0
Watu 11 wamepatikana wamefariki baada ya ndege walioabiri aina ya helikopta kuanguka magharibi mwa mji wa Norway Bergen ikiwa na abiria 13 kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Picha za eneo la mkasa zinaonyesha moshi mkubwa ukifuka kutoka katika mwamba.Ndege hiyo iliharibika vibaya,ripoti zimesema.
Ilikuwa ikipaa kutoka eneo la mafuta la Gullfaks kuelekea mjini Bergen ambacho ni kituo kikubwa cha viwanda vya mafuta ya baharini na gesi.
Msemaji wa polisi Morten Kronen amesema kuwa operesheni kubwa ya uokozi inaendelea ikishirikisha zima moto,waogeleaji na maafisa wa matibabu.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kuwa waliona bawa moja la ndege liking'oka.
''Kulikuwa na mlipuko na sauti mbaya ya mashini ya ndege hiyo kwa hivyo nikachunguza kupitia dirishani''.Nilioona ndege hiyo ikianguka kwa haraka baharini.
''Baadaye nikaona mlipuko mkubwa'',mkaazi mmoja aliliambia gazeti la Bergensavisen.
Vifusi kadhaa vilipatikana katika eneo la nchi kavu huku vyengine vikiwa ndani ya bahari,vyombo vya habari vya eneo hilo vilisema.

Post a Comment

 
Top