0
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo anatarajiwa kumteua Waziri Mkuu, licha ya upinzani ambao ulipaswa kutoa jina hilo, kugawanyika, juu ya nani atakayeteuliwa.
Mpaka sasa upinzani umegawanyika pande mbili, ukiwemo ule unapinga kuteuliwa kwa Felix Tshekedi licha ya kuongoza kundi kubwa na upande mwingine ni wanaomuunga aliyekuwa mshauri mkuu wa marehemu Tsichekedi ambaye alifukuzwa kwenye chama hicho, baada ya kufanya mazungumzo na Rais Kabila.
Hata hivyo kwa mujibu wa rais kabila, kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya ni kutatatua mvutano uliozuka, kuhusi utekelezaji wa makubaliano ya tarehe 31 Desemba mwaka jana, makubalino ambayo yanataka waziri mkuu atoke upande wa Muungano wa upinzani, lakini hadi sasa bado hawaja afikiana kuhusu namna ya kufanya uteuzi, kutokana na mgawanyiko ulitokea upande huo wa upinzani baada ya kifo cha marehemu mkogwe wa upinzani Etienne Tshisekedi, ambae alikuwa anaongoza muungano huu, licha mtoto wake kuteuliwa kuchukuwa nafasi yake hiyo.

Post a Comment

 
Top