Kundi linalotaka kujitenga kwa maeneo ya Basque ETA limethibitisha rasmi taarifa kuwa linapanga kusalimisha silaha Jumamosi tarehe 8. BBC imepata taarifa inayosema kuwa kundi hilo litasalimisha silaha zote na milipuko kupitia wawakilishi wa mashirika ya kijamii.
Punde tu mpango huo utakapo kamilika, hatua hiyo itamaliza ghasia za miongo kadhaa zilizosababisha vifo vya wau zaidi ya 800 na kujeruhiwa kwa maelfu wengine katika kampeni kali ya kundi la ETA katika kupigania uhuru wa Basque katika maeneo ya Uhispania na Ufaransa.
Na iwapo ETA itasalimisha silaha zake itakuwa ndio mwisho wa uasi Ulaya. Kundi hilo linatarajiwa kuvunjika katika miezi inayokuja.
Kwa miongo kadhaa, kundi la ETA lilihusishwana milipuko, mauaji na uporaji. Kwa wafuasi wake ilikuwa ni kupigani uhuru wa Basque, kwa waathiriwa wa ghasia zake, umekuwa muda wa uoga mwingi na kupoteza wapendwa.
Leo eneo la Basque huko Uhispania ni tofuati. Hakujashuhudiwa mashambulio kwamiaka kadhaa na ETA lilitangaza hatua ya kusalimisha silaha mnamo mwaka 2011. Lakini imechukua wakati wote huu kuwashawishi wafuasi wake kufanya hivyo, na kujaribu kusaka silaha zilizosalia.
Taarifa ya ETA hatahivyo inaonya kuwa wale inaowataja kuwa maadui wa amani huenda wakaizuia hatua yao. Lakini duru zilizohusika katika mpango huu zinasema kuna matumaini mpango utatekelezwa katikanamna ambayo itaridhisha na kukubaliwa na pande zote ikiwemo serikali ya Uhispania ambayo daima imekataa kujadiliana na ETA.
Post a Comment