0
Maandamano ya vyama vya upinzani Afrika kusini pamoja na kundi linalo jiita Save South Africa yameanza katika kumshinikiza Rais Jacob Zuma ang'atuke madarakani.
Maandamano hayo yamepangiwa kufanyika nchi nzima.
Wanajeshi wa uMkhonto we Sizwe maarufu MK wametawanywa kushika doria nje ya makao makuu ya chama cha ANC mjini Johannesburg.
Waziri anayeshughulika na masuala ya polisi nchini awali amewaonya wale wote watakao fanya fujo na kuharibu mali ya umma, sheria itafuata mkondo.
wanajeshi MK
Zuma ameponea katika siku za nyuma wito wa kumtaka ajiuzulu.
Aliungwa mkono hivi juzi na kamati kuu ndani ya chama chake cha ANC.
Ilikuwa inachunguza malalamiko yaliowasilishwa na baadhi ya maafisa wa juu wa chama hicho kwamba Jacob Zuma hakushauriana nao kuhusu suala la kufanyia baraza la mawaziri mageuzi.
Shutuma kali zimeibuka kufuatia mageuzi hayo, zaidi kufuatia kutimuliwa kwa waziri wa fedha nchini anayeheshimika na wengi, Pravin Gordhan.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Jeshi la polisi nchini imeeleza kuwa maandamano hayo ya kwenda kwenye ikulu ya Rais hayana kibali, ambacho kimewaruhusu kufika huko.

Post a Comment

 
Top